LONDON, England
WAKALI wa London, Brentford, wako mbioni kukamilisha usajili wa kiungo wa zamani wa Liverpool, Jordan Henderson.
Henderson mwenye umri wa miaka 35, ni mchezaji huru baada ya kuachana na Ajax mwanzoni mwa wiki hii.
Kwa mujibu wa ripoti, nyota huyo atajiunga na Brentford kwa mkataba wa miaka miwili.
Brentford wamemsajili ili kuziba pengo la nahodha wao, Christian Norgaard, ambaye amejiunga na Arsenal.
Kama itakumbukwa, ni miaka 12 imepita tangu Henderson alipoondoka Ligi Kuu ya England mwaka 2023.
Kwa miaka 12 akiwa Anfield, Henderson aliiongoza Liver kutwaa taji la Ligi Kuu kwa mara ya kwanza baada ya kusubiri miaka 30.
Pia, alikuwa sehemu ya kikosi kilichotwaa mataji ya Ligi ya Mabingwa, FA, Kombe la Ligi, Kombe la Dunia kwa ngazi ya Klabu, Uefa Super Cup na Ngao ya Jamii.


