13.1 C
New York

Tyson wa Bongo afunga mtaa, apiga mkwara

Published:

Na Mwandishi Wetu

Bondia wa ngumi za kulipwa Hassan Ndonga maarufu Tyson wa Bongo amefunga  Mtaa wa Banda Mabibo, Dar es Salaam kutokana na wingi wa mashabiki waliojitokeza kumsapoti katika maandalizi ya pambano lake la  Dar Boxing Derby  dhidi ya Mohammed Mpombo  litakalofanyika Julai 26,2025, Viwanja Vya Leaders Club. 

Tyson ambaye anatokea kambi ya Makatuni Pesa, ameweka wazi kuwa hajawahi kufeli katika mapambano yake mengi aliyocheza na kuwahakikishia ushindi mashabiki zake.

“Ukizungumzia K.O huwa inakuja yenyewe ‘automatic, sababu hata ukiangalia mapambano yangu mawili ya mwisho,  la kwanza nilikuwa nacheza raundi nane lakini nikampiga mtu  raundi ya pili, jingine nilicheza Morogoro katika raundi nane nikampiga mpinzani wangu katika raundi ya sita,” ametamba.

Amewaambia mashabiki zake wasisite kujitokeza siku hiyo kwa kuhofia kwani yeye amejipanga  kushinda kutokana na maandalizi anayofanya.

Mmoja wa mashabiki wa bondia huyo,  Hamza. Mohammed, amesema anamkubali bondia wao kwa sababu siku zote hawana kazi mbovu na ameshuhudia hilo mazoezini  na ulingo utasema siku hiyo.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img