LONDON, Uingereza
KATIKA fainali za Kombe la Dunia za mwaka huu (2026) zilizomalizika hivi karibuni, Ferran Torres ndiye aliyefunga bao pekee lililoipa ubingwa timu ya soka ya Hispania katika mechi yao ya fainali dhidi ya Argentina.
Hata hivyo, hatima ya Torres katika kikosi cha Barcelona iko gizani kwani klabu hiyo kwa sasa inahusishwa na straika wa Atletico Madrid, Julian Alvarez.
Je, Torres aliyebakiza mwaka mmoja katika mkataba wake atatimka Camp Nou? Ni klabu ipi anayoweza kujiunga nayo mshambuliaji huyo? Makala haya yanachambua.
PSG
Kocha Luis Enrique anataka kuimarisha kikosi chake katika eneo la ushambuliaji wakati huu Bradley Barcola na Yan Diomande wakiwa njiani kuondoka.
Enrique ndiye aliyempa Torres mechi yake ya kwanza ya timu ya taifa akiwa kocha wa Hispania miaka michache iliyopita.
LIVERPOOL
Majogoo hao wa Anfield wanahitaji kuimarisha eneo la ushambuliaji baada ya Mohamed Salah kufungasha virago vyake na kuondoka mwishoni mwa msimu uliopita (2025-26).
Wakati huo huo, straika raia wa Ufaransa, Hugo Ekitike, ana majeraha yatakayomuweka nje ya uwanja kwa muda mrefu.
REAL MADRID
Kwa wiki za hivi karibuni, Madrid nayo imekuwa ikihusishwa na saini ya Torres. Je, ni rahisi kiasi hicho kwa klabu hizo kufanya biashara?
Mara ya mwisho kwa Barcelona na Madrid kuuziana wachezaji ilikuwa mwaka 2007, ambapo Javier Saviola aliondoka Camp Nou na kutua Santiago Bernabeu.
ASTON VILLA
Kwa kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu (2026-27), Villa ya kocha Unai Emery inahitaji kuboresha kikosi chake ili kuhimili ushindi.
Uzuri ni kamba Villa imevuna mkwanja mrefu, Pauni milioni 117, kwa kumuuza Morgan Rogers aliyejiunga na vigogo wa London, Chelsea.
MANCHESTER CITY
Je, ni wakati sahihi kwa Torres kurejea Etihad? Kama itakumbukwa, Torres alicheza Man City kwa miezi 18, kabla ya kurejea Hispania kujiunga na Barcelona.
Akiwa Man City kwa mwaka mmoja na nusu huo, alifunga mabao 16 katika mechi 43 alizocheza. Pep Guardiola ndiye aliyemfungulia mlango wa kutokea Etihad.


