22 C
New York

Keyshia Cole, Skrilla mambo kwa ushahidi!

Published:

LOS ANGELES, Marekani

PICHA zinazowaonesha mastaa wa muziki Keyshia Cole na Skrilla zimeibua tetesi kuwa huenda wawili hao sasa ni wapenzi.

Katika moja ya picha alizoposti kwenye ukurasa wake wa Instagram, Keyshia ameonekana akiwa bafuni, huku akiwa amemshika kiuno rapa huyo.

Ikumbukwe, ni miaka mitatu tu imepita tangu Keyshia alipohojiwa na jarida la PEOPLE na kusema amekuwa hana bahati kwenye maisha ya mahusiano ya kimapenzi.

Wakati huo, Keyshia alisema shida kubwa ni kwamba wanaume wengi si waaminifu kwenye mahusiano yao. “Wengi ni waongo. Mimi ni mtu ninayependa ukweli,” alisema.

Mwaka jana, mrembo huyo aliyewahi kuolewa na staa wa Ligi Kuu ya Kikapu ya Marekani (NBA), Daniel Gibson, alihusishwa na rapa Hunxho. Katika ndoa yake na Gisbon walipata mtoto mmoja.

Tofauti ya umri siyo ishu kubwa. Kwa sasa, Keyshia ana miaka 44, akimzidi 17 mwanaume wake huyo. Katika baadhi ya picha, wameonekana wakiwa katika ukumbi za starehe.

Related articles

Recent articles