LONDON, Uingereza
KOCHA wa Chelsea, Xabi Alonso, amezipotezea taarifa zinazoihusisha klabu hiyo na usajili wa straika wa zamani wa Arsenal, Danny Welbeck.
Wakati huo huo, Mhispania huyo ameziita kuwa ni tetesi za usajili taarifa zinazodai kwamba wanamtaka kiungo wa zamani wa Liverpool, Jordan Henderson.
Kwa sasa, Welbeck anakipiga Ligi Kuu ya England akiwa na Brighton, wakati huo Anderson anatumikia Brentford.
Alonso amefunga mjadala juu ya kuwataka wachezaji hao baada ya Chelsea kupata ushindi wa mabao 6-4 katika mchezo wa kirafiki wa kujiandaa na msimu ujao (2026-27).
Alipoulizwa kama kikosi cha Blues kinahitaji uzoefu wa nyota hao, alijibu: “Hapana, Nina uhakika tutasikia tetesi nyingi hadi pale dirisha la usajili litakapofungwa.”


