22 C
New York

Vita vinavyozitajirisha kampuni za AI

Published:

Na mwandishi wetu, Gazetini

MSEMO wa ‘vita ni akili’ umedhihirishwa na namna mataifa mengi, hasa makubwa kiuchumi, yanavyotumia akili-unde (Artificial Intelligence – AI) kuwadhibiti wapinzani wake.

Tofauti na kutegemea silaha nzito kama ilivyokuwa miaka mingi iliyopita, sasa vikosi vya majeshi mbalimbali vinaweza kujilinda au kuwashambulia wapinzani pasi na kuwafikia moja kwa moja kwenye uwanja wa vita.

Si tu kujilinda au kushambulia, pia AI imekuwa ikitumiwa na idara za ulinzi katika kufanya maamuzi ya kiusalama kwa ujumla wake.

Tangu Marekani ilipoanzisha utumizi wa Ndege zisizo na rubani katika miaka ya 2000 na 2010, mataifa mengine yamekuwa yakiwekeza mabilioni ya dola katika teknolojia hiyo na zingine.

Kwa ufupi, kampuni kubwa za teknolojia ya AI zimekuwa mnufaikaji mkubwa wa vita vinavyoendelea katika maeneo mbalimbali duniani.

Takwimu zinaeleza kuwa kwa mwaka 2025 pekee, matumizi ya jeshi duniani yalifikia Dola bilioni 2.88, sehemu ya fedha hizo ikielezwa katika ununuzi wa vifaa, programu au mafunzo ya AI.

Julai 10, 2026, Wizara ya Ulinzi ya Uingereza ilisaini mkataba wa miaka 15 wenye thamani ya Dola bilioni 2.7 na kampuni ya Raytheon UK ili wanajeshi wake 600,000 kupatiwa mafunzo ya AI.

Hivi karibuni, Marekani ilisaini mkataba mnono na kampuni nane kubwa duniani za AI, zikiwamo SpaceX na OpenAI, ili kuimarisha mifumo yake ya kujilinda na kushambulia wapinzani.

Aidha, kampuni za AI zinazotajwa kunufaika ziaid na vita vya Ukraine na Urusi na ile ya Marekani dhidi ya Iran ni Anduril, Lockheed Martin Corp, RTX, Northrop Grumman Corp, Palantir, BAE Systems, na General Dynamics Corp.

Related articles

Recent articles