22 C
New York

Umeipata hii? J-Lo ndani ya penzi jipya

Published:

LOS ANGELES, Marekani

BIBIYE mwenye jina na mafanikio makubwa kwenye soko la muziki nchini Marekani, Jennifer Lopez ‘J-Lo’, amenasa kwa mshikaji anayefahamika kwa jina la Keith Urban.

Walianza kwa kujificha lakini kwa sasa siyo siri tena kwani wawili hao wameonekana wakiwa pamoja kwenye mitoko yao mingi ya hivi karibuni.

Chanzo kilichohojiwa na jarida la Heat World UK kimedai kuwa J-Lo mwenye umri wa miaka 57 amechukua nafasi tangu Urban (58) alipoachana na mkewe, Nicole Kidman.

Kabla ya kuingia kwenye uhusiano wa kimapenzi unaoripotiwa kwa sasa, J-Lo na Urban walijuana na kuwa marafiki miaka mingi iliyopita walipokuwa majaji kwenye Shindano la vipaji la American Idol.

Kama ilivyo kwa Urban, J-Lo naye yuko ‘singo” kwani hajaonekana hadharani akiwa na mtu tangu alipoachana na Ben Affleck mwaka 2024.

Related articles

Recent articles