28.6 C
New York

Arsenal bado wamkomalia Guimaraes

Published:

LONDON, Uingereza

ARSENAL hawajarudi nyuma katika mpango wao wa kumsajili nahodha wa kikosi cha Newcastle United, Bruno Guimaraes.

Taarifa zinaeleza kuwa Washika Bunduki wako kwenye meza ya mazungumzo na mabosi wa Newcastle, wakijaribu kuishawishi imwachie Mbrazil huyo.

Arsenal walishaweka mezani ofa yao ya Pauni milioni 70 lakini mabosi wa Newcastle waligoma, wakisema haitoshi kumng’oa kiungo huyo klabuni hapo.

Vyanzo vingine vya habari vimeleza kuwa nyota huyo mwenye umri wa miaka 28 ameonesha kuvutiwa na mpango wa kujiunga na mabingwa hao wa Ligi Kuu ya England msimu uliopita (2025-26).

Aidha, wakati huu mazungumzo yakiendelea, Guimaraes amesafiri na kikosi cha Newcastle kwenda Hispania kwa ajili ya kambi ya msimu ujao (2026-27).

Related articles

Recent articles