NYON, Uswis
MKONGWE wa Arsenal, Arsene Wenger, amekana kuhusika katika uliokuwa mpango wa Rais wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), Gianni Infantino, kuuza hisa za michuano yote ya Taasisi hiyo, ikiwamo Kombe la Dunia.
Infantino alilazimika kuachana na mpango huo baada ya kukosolewa vikali na wadau wa FIFA, likiwamo Shirikisho la Soka la Ulaya (UEFA).
Sasa, wakati huu Infantino akikabiliwa na presha kubwa inayotishia uwezekano wa kushinda Uchaguzi ujao wa mwakani, Wenger ameibuka na kusema hahusiki kwa lolote katika mpango huo wa Infantino.
Na badala yake, Mfaransa huyo ameeleza kuwa kwa nafasi yake, anawajibika zaidi katika shughuli za maendeleo ya soka la vijana ndani ya Shirikisho hilo.
“Pia, nafanya kazi kama mshauri wa ufundi lakini sikushirikishwa juu ya mpango huo (wa kuuza hisa). Kwa mara ya kwanza, niliuona kupita vyombo vya habari,” amesema.


