28.6 C
New York

Caicedo hataki Enzo aondoke Chelsea

Published:

LONDON, Uingereza

KIUNGO wa Chelsea, Moises Caicedo, amekiri kuwa hatamani kuona staa mwenzake, Enzo Fernandez, akiondoka klabuni hapo kama inavyoelezwa na vyombo vya habari.

Caicedo ameeleza hayo katika mahojiano yake mjini Hong Kong, muda mfupi kabla ya Blues kuivaa Juventus katika mchezo wa kirafiki wa kujiandaa na msimu ujao.

Kwa wiki kadhaa sasa, Enzo raia wa Argentina amekuwa akihusishwa na mpango wa kuondoka Stamford Bridge na kutimkia Real Madrid.

“Namkubali sana Enzo,” amesema Caicedo na kuongeza: “Namuheshimu kwa sababu sote tunajua ni mchezaji wa aina gani.

“Sio tu mchezaji, pia ni mtu mzuri. Naamini atabaki lakini sitaki kuzungumzia sana suala hilo. Kama atabaki, litakuwa jambo muhimu sana kwetu.”

Related articles

Recent articles