28.1 C
New York

Chiesa aambiwa aondoke Liverpool

Published:

MERSEYSIDE, Uingereza

KLABU ya Liverpool imemwambia winga wake, Federico Chiesa, kwamba anaweza kuondoka majira haya ya kiangazi na kutafuta timu nyingine.

2025-26 ulikuwa msimu mbaya kwa Chiesa, ambapo aliingia kikosi cha kwanza mara moja pekee katika mechi 26 za Ligi Kuu ya England (EPL) alizocheza.

Kwa upande wake, Chiesa raia wa Italia ameonesha nia ya kubaki Anfield akiamini anaweza kufanya vizuri msimu ujao.

Hata hivyo, Liverpool iko tayari kukaa mezani na klabu yoyote itakayofika mezani na kitita cha Pauni milioni 15.

Chiesa aliyebakiza miaka miwili katika mkataba wake na Liverpool, alisajiliwa mwaka 2024 akitokea Juventus ya Serie A.

Related articles

Recent articles