24.3 C
New York

Jordan wabahatika kupishana na Messi

Published:

MEXICO CITY, Mexico

KOCHA wa timu ya soka ya Taifa ya Argentina, Lionel Scaloni, amethibitisha kuwa atampumzisha nahodha wake, Lionel Messi, katika mchezo wao dhidi ya Jordan.

Timu hizo zitakutana kesho Juni 28, 2026, ukiwa ni mchezo wa mwisho wa kundi lao lenye timu zingine mbili, Algeria na Austria.

Argentina ikiwa imeshavuka makundi, ni wazi haitoyatolea macho matokeo ya mechi hiyo na ndiyo maana Messi atapumzika kujiandaa na hatua ya 32 Bora.

“Matumaini ni kuona timu ikicheza vile vile. Ndicho tunachotaka kujaribu kukifanya,” amesema.

Hata hivyo, kocha huyo aliyeipa Argentina ubingwa wa Kombe la Dunia mwaka 2022, amesema hawaichukulii poa Jordan, na badala yake watakabiliana nayo kama timu bora.

Related articles

Recent articles