27 C
New York

Aziz Ki, Okello, Pacome, Dube: Kombinesheni ya ‘asali na maziwa’ Yanga?

Published:

Na mwandishi wetu, Gazetini

TETESI zimezidi kushika kasi juu ya uwezekano wa kiungo wa kimataifa wa Burkina Faso, Stephanie Aziz Ki, kurudi Yanga kwa ajili ya msimu ujao (2026-27).

Ripoti hizo ziliongezwa kasi na kitendo cha Aziz Ki kuonekana jukwaani wakati Yanga ikimenyana na TRA United jana Juni 27, 2026.

Taarifa ambazo si Yanga wala Aziz Ki aliyethibitisha, zinadai kuwa klabu hiyo imeshawasilisha ofa yao kwa Al-Ittihad ya Libya ili imwachie.

Kwa mashabiki wa Yanga, taarifa za kurudi kwa ‘fundi’ huyo zinakuja wakati huu safu yao ya ushambuliaji ikiwa inabebwa na staa wa Uganda, Allan Okello, akishirikiana na Pacome Zouzoua na Prince Dube.

Aidha, mashabiki wanaamini kuwa endapo Aziz Ki atasajiliwa na kuungana nao, safu ya ushambuliaji ya Yanga itakuwa moto wa kuotea mbali.

Aziz Ki si jina geni nchini, akifahamika kwa uwezo wake wa kutengeneza nafasi, kupiga mashuti ya mbali, kutoa ‘asisti’, na hata kufunga mabao.

Hivyo, picha wanayoipata mashabiki ni hii; Aziz Ki na Okello watokee (winga ya kulia na kushoto), Zouzoua acheze namba 10, kisha Prince Dube asimame (namba 9).

Pia, ipo picha nyingine; Pacome na Okello watokee pembeni (kulia na kushoto), kisha Aziz Ki atulie namba 10, yaani acheze nyuma ya straika Dube.

Faida iliyopo kwa nyota hao, mbali ya uwezo mkubwa wa kufunga, pia kila mmoja ni mzuri katika kutengeneza nafasi kwa wenzake.

Lakini je, ni kweli Aziz Ki atarudi Jangwani baada ya misimu michache kupita tangu alipoondoka na kujiunga na Wydad Casablanca ya Morocco, kabla ya kutua Al-Ittihad?

Related articles

Recent articles