LONDON, Uingereza
NAHODHA wa Sunderland na timu ya soka ya Taifa ya Uswis, Granit Xhaka, huenda akajiunga na Chelsea kupitia dirisha kubwa ma majira haya ya kiangazi.
Kwa mujibu wa Gazeti la Daily Mail la Uingereza, kocha mpya wa Chelsea, Xabi Alonso, ndiye aliyependekeza usajili wa Xhaka.
Hata hivyo, mabosi wa Sunderland wamesisitiza kuwa kiungo huyo wa zamani wa Arsenal hauzwi.
Xhaka aliwahi kufanya kazi na Alonso wakati huo kocha huyo akiwa kocha wa Bayern Leverkusen ya Bundesliga.
Alonso anaamini nyota huyo mwenye umri wa miaka 34 ataongeza uzoefu katika kikosi chake cha msimu ujao (2026-27).
Nyota huyo ana mkataba na Sunderland utakaokwisha mwaka 2028 lakini ameonesha nia ya kumfuata Alonso pale Stamford Bridge.


