TORONTO, Canada
STRAIKA Harry Kane ameandika historia mpya baada ya kuwa mfungaji bora wa muda wote wa timu ya soka ya Taifa ya England katika michuano ya Kombe la Dunia.
Kane ameweka rekodi hiyo baada ya kufikisha mabao 11, akimzidi moja lejendari wa timu hiyo, Gary Lineker.
Nyota huyo wa Bayern Munich amefikia idadi hiyo baada ya kufunga moja katika ushindi wa mabao 2-0 walioupata England mbele ya Panama.
Amefikisha mabao 11 katika mechi 14 za Kombe la Dunia, wakati Lineker alifunga 10 kwa mechi 12.
Anayefuata katika nafasi ya tatu kwa kuifungia England mabao mengi kwenye Kombe la Dunia ni Geoff Hurst mwenye matano, na Bobby Charlton, Michael Owen na Marcus Rashford, kila mmoja akiwa na manne.
Wengine wenye mabao matatu ni
David Beckham, Steven Gerrard, Roger Hunt, David Platt, Bukayo Saka, na
Nat Lofthouse.


