Na mwandishi wetu, Gazetini
KATIKA sehemu ya pili ya makala haya,tuliona Lungu akipoteza kiti cha urais mbele ya mpinzani wake, Hichilema, ambaye awali alimshinda mara mbili (2015 na 2016).
Safari hii, walikutana katika Uchaguzi wa mwaka 2021, ambapo Lungu alishindwa kurudi madarakani na kumpisha Hichilema wa Chama cha upinzani cha UNPD.
Pia, tuliona Lungu akikubaliana na matokeo, hatua iliyofuatiwa na uamuzi wake wa kustaafu siasa za ushindani, ikiwa ni pamoja na kujiuzulu nafasi yake ya Rais wa Chama cha Patriotic Front (PF). Endelea kusoma …
Mei 3, 2023, polisi walifika nyumbani kwa Lungu na kufanya ukaguzi, ikielezwa kuwa mkewe alikuwa akimiliki baadhi ya magari kwa njia zisizo halali.
Miezi michache baadaye, Lungu aliitangaza kurudi kwenye ulingo wa siasa na kushika tena nafasi ya Rais wa Patriotic Front (PF), ingawa hatua hiyo ilisababisha mpasuko mkubwa ndani ya Chama hicho.
Chama kikagawanyika pande mbili; moja ikimtambua Miles Sampa kama Rais, na nyingine ikimuunga mkono Lungu kwenye nafasi hiyo hiyo.
Katikati ya mvutano, Lungu aliamua kujiondoa na kujiunga na Muungano wa vyama vya upinzani, United Kwacha Alliance (UKA), mwanzoni mwa mwaka 2024.
Kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2026, Lungu aliondoka UKA na kujiunga na New Congress Party (NCP) kilichopanga kumteua kuwa mwakilishi wake kwenye kinyang’anyiro cha urais.
Hata hivyo, ndoto hiyo ilizimwa na Mahakama ya Katiba ya Zambia iliootangaza Desemba 10, 2024, kwamba Lungu hapaswi kugombea tena kwani tayari alishakuwa Rais wa Zambia kwa awamu mbili (2015-16 na 2016-21).
Mwaka 2025, Miles Sampa aliamua kumaliza mgogoro wa muda mrefu ndani ya Chama cha PF kwa uamuzi wake wa kumkabidhi Lungu kiti cha urais.
Je, nini kutafuta? Katika sehemu ya nne inayofuata, tutagusa maisha binafsi, maradhi na hata kifo cha kiongozi huyo; Rais wa zamani wa Zambia, Edgar Lungu, ambaye bado hajazikwa, licha ya kufariki mwaka mmoja uliopita.
Usikose tafadhali.


