17.4 C
New York

Rihanna alivyozama mazima penzi la A$AP Rocky

Published:

LOS ANGELES, Marekani

MIAKA mitano iliyopita, ndipo wanamuziki wawili maarufu, Rihanna na A$AP Rocky, walipoianza safari yao ya mapenzi iliyozalisha familia ya baba, mama na watoto watatu.

Walianza kama marafiki wa kikazi, ambapo rapa A$AP alikuwa sehemu ya ziara ya Rihanna ya Diamond Tour mwaka 2013, kisha kumtumia bibiye huyo kwenye video ya wimbo wake maarufu wa ‘Fashion Killa’.

Minong’ono ya wawili hao kuwa wapinzani ilianza kusikika kama utani Januari, 2020, baada ya Rihanna kuachana na bilionea Hassan Jameel.

Kabla ya hapo, A$AP alikuwa kwenye uhusiano uliodumu mwaka mmoja (2016-2017) na bibiye anayetoka familia ya mastaa ya Kardashian, Kendall Jenner.

Kuvuma kwa taarifa za Rihhna na A$AP kulikuja baada ya wawili hao kuripotiwa kuonekana wakiwa pamoja kwenye Tamasha la Yams Day Benefit mjini Brooklyn.

Licha ya vyanzo vingine vya habari kukanusha, walionekana tena pamoja kwenye tangazo la kampuni ya vipodozi ya Rihanna, kisha wakanaswa tena wakiwa na marafiki zao mjini New York.

Hata hivyo, mambo yalionekana ‘siriaz’ zaidi Desemba, 2020, baada ya A$AP kwenda Barbados alikozaliwa Rihanna na wawili hao kusherehekea pamoja Sikukuu ya Krismas.

Mei, 2021, kwa mara ya kwanza, mshikaji alifunguka juu ya uhusiano wake na Rihanna akimtaja kuwa ndiye ‘mrembo na mpenzi wa maisha’ yake.

Kuanzia hapo, ni kama kapo hiyo iliona hakuna tena haja ya kujificha. Januari, 2022, walifichua kuwa ni wazazi watarajiwa na siku chache baadaye Rihanna aliwaonesha tumbo maparazi.

Machi, 2022, akiwa kwenye manunuzi ya nguo za mtoto atakayezaliwa, Rihanna alinaswa akiwa na pete ya uchumba, hivyo kuibua minong’ono kuwa huenda ndoa ilikuwa njiani.

Mtoto wao wa kwanza, RZA, alizaliwa miezi miwili baadaye, kisha mwingine aitwaye Riot akazaliwa Agosti, 2023, kabla ya binti wao pekee, Rocki Irish, kuzaliwa mwaka 2025.

Related articles

Recent articles