17.4 C
New York

Kumbe wanamuziki hawalipwi kutumbuiza Kombe la Dunia

Published:

MEXICO CITY, Mexico

KUTUMBUIZA katika ufunguzi wa Kombe la Dunia, kama walivyofanya Shakira na Burna Boy, kunaweza kutafsiriwa kuwa ni dili linalowapa pesa nyingi wanamuziki wanaobahatika kuitwa.

Kinyume chake, ni dili lisilohusisha malipo ya fedha, na badala yake ni jukwaa la msanii kujiongezea mafanikio, heshima na kuandika historia.

Kwa msanii, atapata faida ya kujitangaza, hivyo kuongezeko mauzo ya albamu na idadi ya watu wanaomfuatilia kwenye majukwaa ya kidigitali.

Ni kwa maana hiyo, mwanamuziki anaweza kukataa mwaliko wa kutumbuiza katika hafla ya fainali za Kombe la Dunia endapo ataona inafaa kufanya hivyo. Siyo lazima kwenda.

Kwa upande mwingine, msanii hatohusika katika gharama za usafiri, mathalan Burna Boy kutoka Nigeria hadi Mexico, na badala yake Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) litasimamia hilo.

Pia, kama iliyotokea kwa Shakira kuandaa wimbo maalumu wa msimu huu, uitwao ‘Dai Dai’, staa huyo wa Pop hakuhusika katika gharama za kurekodi. FIFA ndiyo iliyogharamia.

Related articles

Recent articles