26.6 C
New York

Ndoa ya Taylor Swift inavyoitikisa Marekani

Published:

LOS ANGELES, Marekani

GUMZO kubwa katika tasnia ya burudani nchini Marekani ni ndoa ya bibiye Taylor Swift na mpenzi wake, Travis Kelce, huku mashabiki wa ‘kapo’ hiyo wakibaki njiapanda juu ya siku ya sherehe hiyo.

Swift, mwanamuziki tajiri wa Pop, na Kelce walitangaza rasmi kuwa kwenye uhusiano mwaka 2023 na tangu hapo wamekuwa na ushawishi wa kutosha kwenye tasnia ya burudani.

UTATA WA SIKU YA NDOA

Kwa sababu za usalama, mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 36 hajaweka wazi siku ya ndoa na hiyo na katika kuhakikisha inabaki kuwa siri wageni wamealikwa kwa kupigiwa simu na si kupewa kadi za mwaliko.

Kwa sasa, mashabiki wake wamebaki wakihisi tu, wengine wakisema itakuwa Desemba 13, 2026 kwa kuwa ndiyo siku ya ‘birthday’ yake.

Pia, wengine wanasema bibiye huyo ataolewa Juni 13, 2026. Ni kwa sababu ndoa nyingi nchini Marekani hufungwa Juni, ambacho ni kipindi cha majira ya joto.

Wapo pia wanaoamini kuwa ndoa itafungwa Julai 3, 2026, Siku ya kumbukizi ya miaka 250 ya Uhuru wa Marekani. Swift ni mpenzi wa Siku hiyo na amekuwa akiandaa sherehe binafsi kila mwaka nyumbani kwake.

Tarehe hiyo imetajwa pia na mtandao maarufu na unaoaminika kwa habari za burudani na maisha ya mastaa nchini Marekani, TMZ.

ITAFANYIKA WAPI?

Pia, kwa sababu za usalama, Swift hajasema chochote juu ya watakakofungia ndoa. Je, ni katika moja ya mijengo anayomiliki katika miji mikubwa ya London, New York City na Nashville?

Jijini New York, Ukumbi wa Madison Square Garden unaopokea wageni 22,000 nao unatajwa kutokana na kiwango chake kizuri cha usalama.

Pia, ukumbi huo ambao Swift amewahi kufanya shoo kubwa nyingi, una maegesho ya magari yaliyojificha, hivyo ni rahisi kwa watu maarufu kuingia na kutoka bila kukutana na raia.

Wakati huo huo, huenda pia ndoa ikafungiwa Missouri, Mji ambao Swift na Kelces walikutana kwa mara ya kwanza. Pia, Swift anatokea Pennsylvania na Kelces ni mzaliwa wa Ohio, hivyo moja ya maeneo hayo linaweza kutumika.

MTOKO WA MASTAA

Kwa mujibu wa taarifa, ambazo hata hivyo hazijathibitishwa na Swift wala Kelces, sherehe ya ndoa yao itahudhuriwa na wageni 1,200, wakiwamo marafiki zake wakubwa, Selena Gomez na Jack Antonoff.

Mwanamuziki Benson Boone na mwigizaji Suki Waterhouse nao wamethibitisha kualikwa na watakuwepo, licha ya kutotaja siku ya harusi.

Mwanamitindo Karlie Kloss na mwimbaji Benson Boone nao watakuwepo, kama ilivyo kwa mwigizaji Miles Teller na mkewe, Keleigh Sperry Teller.

Tofauti na sherehe zingine za mastaa, mwaliko wa Swift haujaweka nafasi ya mtu wa ziada. Kwamba kama amealikwa Selena Gomez peke yake, basi asiongozane na mtu mwingine., akiwamo mume wake, Benny Blanco.

Related articles

Recent articles