27.2 C
New York

Meli ya mizigo yazama, watu 23 hawajulikani walipo

Published:

BEIJING, China

MELI ya mizigo ya Vietnam imeripotiwa kuzama jirani na Mwamba wa Yongshu katika Bahari ya South China.

Vyombo vya habari vya China vimeripotiwa taarifa hiyo, vikieleza kuwa timu ya uokoaji inaendelea kutafuta wafanyakazi 23 kati ya 62 waliokuwa kwenye meli hiyo.

Aidha, mamlaka za Jimbo la Hainan zimeeleza kuwa meli iliyozama ni aina ya Khoi ​Nguyen 18 na ilizama baada ya kupata hitilafu ikiwa umbali mfupi kutoka ulipo Mwamba wa Yongshu.

Wakati huo huo, taarifa ya mamlaka zimedai kuwa meli ilikuwa na wafanyakazi 62 lakini 39 wamweshaokolewa, hivyo 23 hawajulikani waliko.

Kwa upande wake, Shirika la Utangazaji la China, Xinhua, limeeleza kuwa meli hiyo ya Khoi Nguyen 18 ilikuwa na urefu wa meta 70, sawa na futi 230.

Related articles

Recent articles