LONDON, Uingereza
KLABU ya Arsenal imekamilisha usajili wa kiungo wa Cardiff City, Axel Donczew, ambaye ni ‘bwana mdogo’ mwenye umri wa miaka 16.
Kwa mujibu wa ripoti mpya kutoka Italia, Donczew amefanya vipimo na dili lake litatangazwa siku chache zijazo.
Aliyefichua uwepo wa dili hilo ni mwandishi wa habari za michezo maarufu wa Italia, Fabrizio Romano, kupitia ukurasa wake wa X.
Katika taarifa yake kwenye mtandao huo, Romano ameandika: “Arsenal imekubali usajili wa kinda wa miaka 16 katika klabu ya Cardiff City, Axel Donczew.”
Donczew anacheza eneo la kiungo mshambuliaji na tayari ameshaanza kutumikia timu za vijana za Wales kuanzia U-15 na U-19.


