MADRID, Hispania
MWANAMUZIKI maarufu wa Pop raia wa Colombia, Shakira, ameeleza alivyopitia wakati mgumu baada ya kuachana na mwanasoka Gerrard Pique mwaka 2022.
Katika mahojiano ya hivi karibuni, Shakira amesema kuachana na Pique kulimpa wakati mgumu zaidi kuwahi kuwa nao katika maisha yake.
“Nilijiona dhaifu kuliko kipindi chote cha maisha yangu,” amesema Shakira, ambaye alikuwa na Pique kwenye uhusiano uliodumu kwa miaka 11.
Shakira na Pique waliachana wakiwa wamebahatika kupata watoto wawili, Milan (miaka 13) na Sasha (miaka 11).
Bibiye huyo amesema kwa sasa anaendelea vizuri katika malezi ya watoto wake wawili alioachiwa na beki huyo wa zamani wa Barcelona na timu ya Taifa ya Hispania.


