25 C
New York

Lil Wayne anasa kwa ‘kitoto cha 2000’

Published:

LOS ANGELES, Marekani

BAADA ya Lil Wayne kuachana na mpenzi wake wa muda mrefu, Denise Bidot, staa huyo wa muziki wa Hip hop ameripotiwa kuangukia kwa binti mwenye umri usiozidi miaka 20.

Wayne (43), ambaye jina lake halisi ni Dwayne Michael Carter Jr, ndiye aliyemtema Bidot baada ya kumtumia bibiye huyo meseji ya kuachana.

Kwa mujibu wa mtandao maarufu wa habari za mastaa wa TMZ, kwa sasa Wayne anatokana na mrembo huyo anayeishi Indiana.

Kabla ya kuwa na Bidot, rapa huyo wa ngoma maarufu ya ‘Lollipop’ alikuwa na mwanamitindo La’Tecia Thomas, ambaye waliachana mwaka 2020.

Ifahamike kuwa supastaa huyo ni baba wa watoto watano katika mahusiano na wanawake tofauti, akiwamo Bidot aliyepata naye mtoto mmoja wa kike.

Nje ya hapo, mmoja ya watoto wake wa kiume anaitwa Neal, ambaye alimpata katika uhusiano na mwanamuziki mwenzake, Nivea.

Aliwahi pia ‘kupita’ na mrembo Lauren London na mtangazaji wa vipindi vya redio, Sarah Vivan, na kupata watoto wawili wa kiume, kisha binti aitwaye Reginae Carter katika ndoa yake na Toya Johnson.

Related articles

Recent articles