23.1 C
New York

Ufaransa v Hispania: Nusu fainali ya heshima Kombe la Dunia 2026

Published:

TEXAS, Marekani

TIMU ya soka ya Taifa ya Ufaransa itamenyana na Hispania katika mchezo wa nusu fainali ya msimu huu wa Kombe la Dunia. Mechi itachezwa Julai 14, 2026 mjini Texas.

Ufaransa ‘Les Bleus’ ni mabingwa wa Kombe la Dunia mwaka 2018, wakati Hispania ni mabingwa wa fainali za EURO za mwaka 2024. Patamu hapo!

Ufaransa imetinga nusu fainali ikiwa imeshinda mechi zote sita za msimu huu wa Kombe la Dunia.

Katika hatua ya robo fainali, walikutana na vigogo wa soka la Afrika, Morocco, lakini walivuka kwa ushindi safi wa mabao 2-0.

Jeuri yao kwenye michuano hii iko kwa mshambuliaji wao tishio, Kylian Mbappe, ambaye tayari ana mabao nane katika michezo sita.

Hii ni nusu fainali ya tatu mfululizo kwa Ufaransa kwenye mashindano haya ya Kombe la Dunia baada ya kufika hatua hii mwaka 2018 na 2022. Walifika fainali mara zote hizo.

Hispania, kwa upande wao, hii ni nusu fainali yao ya kwanza ya Kombe la Dunia tangu walipotwaa ubingwa wa michuano hiyo mwaka 2010.

‘La Roja’ walivuka robo fainali kwa ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Ubelgiji. Aliyeokoa jahazi ni Mikel Merino aliyefunga bao la ushindi, kama alivyofanya katika mchezo uliopita wa hatua ya 16 Bora dhidi ya Ureno.

Related articles

Recent articles