MIAMI, Marekani
NYOTA wanne kwa sasa ndiyo wanaokabana koo katika kuiwania tuzo ya mwaka 2026 ya Ballon d’Or kuelekea mchezo wa fainali ya Kombe la Dunia.
Nahodha wa timu ya soka ya Taifa ya Argentina, Lionel Messi, ambaye atakwaana na England katika fainali, ni miongoni mwa wanaopewa nafasi kubwa.
Messi aliyetoa asisti mbili katika ushindi wa 2-1 dhidi ya England, anapewa asilimia 31.7, kwa mujibu wa mtandao wa Polymarket.
Katika nafasi ya pili, ni mshambuliaji wa Hispania, Lamine Yamal, mwenye asilimia 30.9, akifuatiwa na nahodha wa England, Harry Kane (13.5%).
Wakati huo huo, staa wa timu ya Taifa ya Ufaransa na klabu ya PSG, Ousmane Dembele, naye yumo akiwa na asilimia 3.1.
Ifahamike kuwa tuzo ya mshindi wa Ballon d’Or inatarajiwa kutolewa Oktoba 26, 2026.


