13.5 C
New York

WB: Vita vya Iran vinayaachia madeni Afrika

Published:

NEW YORK, Marekani

BENKI ya Dunia (WB) imeeleza kuwa vita vya Iran vimezifanya nchi nyingi za Afrika kukopa fedha ili kukabiliana na dharura ya kiuchumi.

Vita hivyo vilianza Februari, 2026, kwa matumaini ya kumalizika ndani ya muda mfupi lakini vimeendelea kwa miezi mitatu sasa, huku dalili za kumalizika zikiwa bado hazijaonekana.

Kwa mujibu wa WB, mataifa 27 barani Afrika yamebisha hodi na kuchukua mkopo tangu Iran ilipoanza vita yake na Marekani inayoshirikiana na Israel.

Kenya ni miongoni mwa nchi zilizoomba msaada wa dharura kutoka WB ili kukabilana na changamoto ya kupanda kwa bei ya nishati ya mafuta.

“Mgogoro huo umeathiri soko la nishati duniani. Mathalan, usafirishaji wa meli za mbolea kwenda katika nchi zinazoendelea (Afrika) umeathirika,” imeeleza taarifa ya WB.

Katika hatua nyingine, WB imeahidi kutenga kiasi cha Dola bilioni 25 kwa ajili ya kuzipa nchi zinazohitaji msaada wa dharura kutokana na kinachoendelea Mashariki ya Kati.

Related articles

Recent articles