15.6 C
New York

Mkakati wa kutokomeza saratani ya kizazi

Published:

EDINBURGH, Scotland

SARATANI ya kizazi ni moja ya saratani nne zinazotesa wanawake duniani, ikihusishwa pia na vifo vingi kwa jinsia hiyo.

Hata hivyo, hadithi ni tofauti nchini Scotland, ambako mikakati wa chanjo kuanzia kwa mabinti wenye umri wa miaka 12 umeonekana kuzaa matunda.

Kwa mujibu wa utafiti wa vyuo vikuu vya Strathclyde na Edinburgh, chanjo hiyo imeifanya Scotland ifanikiwe katika mpango wake wa kutokomeza saratani ya kizazi.

Mpango huo ulioanza mwaka 2019, unaanzia shuleni, ukihusisha kuwapa chanjo wanafunzi wenye wa kike na wa kiume wenye umri kati ya miaka 12 na 13.

Mpango huo unawezesha kuwapatia chanjo asilimia 80 ya wanafunzi wanaomaliza kidato cha nne kila mwaka, wakati huo wakiwa na umri kati ya miaka 15-16.

Kwa barani Ulaya, dozi ya kwanza ya chanjo ya saratani ya kizazi kwa vijana wenye umri wa miaka 15 ilitekelezeka kwa asilimia 40 mwaka 2023.

Saratani ya kizazi huchukua miaka 10 hadi 20 kwa dalili zake kuanza kujitokeza. Tafiti zinaonesha kuwa mwanamke huanza kuonesha dalili akiwa na umri kati ya miaka 30 hadi 34.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img