9.5 C
New York

Jengo la kanisa laua watatu, waziri afunguka

Published:

ACCRA, Ghana

WATU watatu, wakiwamo wanawake wawili, wameripotiwa kupoteza maisha baada ya jengo la ghorofa mbili la kanisa kuporomoka mjini Accra.

Waziri wa Mambo ya Ndani, Muntaka Mohammed-Mubarak, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo jana Machi 29, 2026.

Kwa mujibu wa Waziri huyo, wengine 20, wakiwamo watoto, wameokolewa na wanaendelea na matibabu katika hospitali mbalimbali.

Hata hivyo, chanzo cha kuporomoka kwa jengo hilo la ghorofa mbili hakijafahamika, ingawa ajali ilitanguliwa na mvua mkubwa iliyoyesha.

Wakati huu uchunguzi ukiendelea, taarifa zinaeleza kuwa jengo hilo halikuwa limekamilika katika ujenzi.

“Tunachoweza kusema ni kwamba kulikuwa na jumla ya watu 23 … Ni siku mbaya kwetu sote,” amesema Waziri Mohammed-Mubarak.

Kwa upande wao, raia na wakazi wa eneo hilo wameelekeza lawama zao kwa mamlaka wakisema tukio hilo ni matokeo ya uzembe.

“Hakuna asiyejua kuwa jengo lilikuwa dhaifu, lakini bado mamlaka ziliruhusu shughuli kufanyika,” amesema mmoja ya mashuhuda.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img