Na mwandishi wetu, Gazetini
TANZANIA inaendelea kupiga hatua katika upatikanaji wa huduma za mawasiliano kupitia teknolojia mbalimbali za mitandao ya simu.
Kwa mujibu wa ripoti ya karibuni iliyotolewa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), teknolojia ya 2G inafikia takribani asilimia 98.6 ya wananchi, huku 3G ikifikia asilimia 93.8 na 4G asilimia 94.2.
Aidha, teknolojia ya 5G inaendelea kuongezeka ambapo sasa inafikia asilimia 28 ya watu, ikipanda kutoka asilimia 26 iliyorekodiwa mwezi Juni 2025.
Ukuaji huo unaonyesha juhudi za kuimarisha miundombinu ya mawasiliano nchini, huku wananchi wengi zaidi wakipata fursa ya kutumia teknolojia za kisasa za intaneti.


