24.4 C
New York

Liverpool yamaliza vibaya ‘pre-season’

Published:

CHICAGO, Marekani

LIVERPOOL chini ya kocha mpya, Andoni Iraola, imetandikwa mabao 4-2 na Leeds United katika mchezo wao wa mwisho wa maandalizi ya msimu ujao wa 2026-27.

Mbaya Zaidi kwa Liverpool, waliruhusu mabao manne hayo ndani ya dakika 25 za mchezo hupo uliochezwa jana Agosti 2, 2026, mjini Chicago.

Kabla ya kupimana ubavu na Leeds, Liverpool ilicheza mechi zingine mbili za kirafiki, ambazo ilishinda zote kwa ushindi wa jumla ya mabao 5-2.

Katika mchezo wa kwanza uliochezwa Julai 25, 2026 nchini England, ‘Majogoo’ waliondoka na ushindi mnono wa mabao 4-2 dhidi ya Sunderland.

Mechi yao iliyofuata ni ya Julai 30, 2026, ambapo Liverpool walikuwa mjini New York na kushinda bao 1-0 dhidi ya Wrexham.

Related articles

Recent articles