8.9 C
New York

Morocco kutumia Bil. 858/- kukabiliana na mafuriko

Published:

CASABLANCA, Morocco

SERIKALI ya Morocco imepanga kutumia kiasi cha Dola milioni 330 (zaidi ya Sh bil. 858 za Tanzania) kukabiliana na uharibifu uliosababishwa na mafuriko.

Hatua hiyo ni utekelezaji wa agizo la Mfalme wa nchi hiyo, Mohammed VI, aliyeteka kuwapo kwa programu ya kuiwezesha familia na jamii zilizoathirika.

Majimbo manne ya Larache, Kenitra, Sidi Kacem na Sidi Slimane yametajwa kuathiriwa zaidi, hivyo Dola milioni 328 zitaelekezwa huko.

Mbali ya kuharibu makazi na maeneo ya biashara, pia mafuriko hayo yameiacha kwenye hali mbaya miundombinu ya usafiri na kilimo.

Mafuriko yameiathiri Morocco tangu mwishoni mwa Januari, 2026, ambapo watu takribani 188,000 wameachwa bila makazi katika maeneo mbalimbali.

Katika tukio la hivi karibuni, watu wanne walipoteza maisha baada ya gari walilokuwamo kusombwa na mafuriko.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img