MOSCOW, Urusi
SERIKALI ya Urusi imeagiza kufutwa kwa matumizi ya WhatsApp nchini humo, huku ikiwa na mbadala wa mtandao huo wa kijamii.
Mamkala zimetoa agizo hilo ili mtandao mpya aina ya WhatsApp, ambao ni mali ya Serikali, uweze kutumika.
Kwa upande wake, Kampuni ya Meta, ambayo ndiyo wamiliki wa WhatsApp, imelaani mpango huo na kusema utawaondoshea wateja wake zaidi ya milioni 100 walioko Urusi.
Lakini, kwa mujibu wa Msemaji wa Serikali ya Kremlin, Dmitry Peskov, uamuzi huo umetokana na Meta kushindwa kukubaliana na baadhi ya masharti.
Kile kilichoelezwa na Peskov ni kwamba walikaa mezani na Meta lakini kampuni hiyo haikuweza kukubaliana na tamaduni na sheria za Urusi.
Ameongeza: “Meta inaweza kuendelea na huduma za endapo itakubaliana na hayo katika mazungumzo.”


