22 C
New York

Apple yaiburuza Samsung mauzo ya simu

Published:

BEIJING, China

BAADA ya miaka 14 ya kuwa nyuma ya Samsung kwa mauzo ya simu, kampuni ya Apple imeamka na kushika nafasi ya kwanza duniani.

Kwa mujibu wa utafiti wa Taasisi ya Counterpoint Research ya Hong Kong, Apple ilipata asilimia 20 ya usafirishaji wa simu duniani kote kwa mwaka jana.

Kwa kufanya hivyo, waliipiku Samsung, ambayo kwa mwaka jana ilipata asilimia 19 ya usafirishaji wa simu duniani.

Samsung ya Korea Kusini, imekuwa kinara wa uuzaji wa simu duniani kwa miaka 14, kabla ya Apple sasa kushika nafasi hiyo.

Kwa mujibu wa utafiti wa Counterpoint Research, faida kubwa waliyonayo Aple ni gharama nafuu ya simu zao, ukilinganisha na Samsung.

Akizungumzia ushindani uliopo kati ya kampuni hizo, mtaalamu wa masoko wa Counterpoint Research, Yang Wang, Samsung wanapaswa kujifunza kwa Apple kwa kushuka na kuwafia wateja wa kipato cha kawaida.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img