MILAN, Italia
IKIWA ni miaka 11 imepita tangu alipotangaza kustaafu, kiungo wa zamani wa Barcelona, Ronaldinho, amerejea dimbani.
Ronaldinho (46), amesajiliwa na klabu ya Ravenna inayoshiriki michuano ya Ligi Daraja la Tatu nchini Italia (Serie C).
Kwa mujibu wa ripoti, nyota huyo aliyekuwa sehemu ya kikosi cha timu ya Taifa ya Brazil kilichotwaa Kombe la Dunia mwaka 2002, atatambulishwa rasmi wiki ijayo.
“Nasubiri kwa hamu kuchezea mpira na kuandika historia mpya …” ameandika ‘Gaucho’ katika kurasa zake za mitandao ya kijamii.
Klabu yake mpya iko Kaskazini mwa Italia na uwanja wake wa nyumbani ni Bruno Benelli.
Aidha, klabu hiyo haiko mbali na masikani ya Bologna inayoshiriki Ligi Kuu ya Italia (Serie A).


