27.9 C
New York

Iran yafunga tena Hormuz, yaitaja Israel

Published:

TEHRAN, Iran

MAMLAKA za Iran zimetangaza hatua yake ya kuufunga kwa mara nyingine Mlango-Bahari wa Hormuz, huku ikilaani mashambulizi ya Israel nchini Lebabon.

Hatua hiyo ya Iran inakuja licha ya kutangaza kuufungua Mlango-Bahari huo baada ya makubaliano yake na Marekani.

Hormuz ni njia maji inayopitisha asilimia 20 ya meli za mafuta na gesi zinazoingia kwenye soko la dunia.

Awali, Iran iliufunga na kusababisha adha kubwa ya uhaba na kupanda kwa bei ya nishati hizo duniani kote.

Iran inataka makubaliano ya kusitisha vita kati yake na Marekani yaheshimu pia usalama wa Lebanon.

Hata hivyo, Israel imetekeleza mashambulizi kadhaa Kusini mwa Lebabo na kusababisha vifo vya watu takribani 32.

Related articles

Recent articles