MEXICO CITY, Mexico
JAPAN na Tunisia zitavaana Jumapili ya Julai 21, 2026 katika mchezo wa Kundi F msimu huu wa fainali za Kombe la Dunia.
Upekee wake ni kwamba hiyo itakuwa mechi ya 1,000 ya michuano hiyo tangu ilipoanzishwa mwaka 1930.
Timu hizo zitakwaana kwenye Uwanja wa Mexico, kila moja ikicheza mechi yake ya pili msimu huu wa Kombe la Dunia.
Kwa upande wao, Japan watarejea dimbani baada ya sare ya mabao 2-2 waliyoipata mbele ya Uholanzi katika mechi yao ya kwanza, wakati Tunisia walifungwa mabao 5-1 na Sweden.
Kocha wa Japan, Hajime Moriyasu, amesema mechi ya 1,000 ina maana kubwa kwao kuhakikisha wanawafunga Tunisia.
Nahodha wa Tunisia, Ellyes Skhiri, naye amesema mechi hiyo ina ujumbe wa heshima kwa wachezaji wote wa timu hiyo, hivyo wanapaswa kuimaliza kwa ushindi.


