Na mwandishi wetu, Gazetini
SIMBA SC imekuwa ya kwanza kutanguliza mguu fainali ya Kombe la FA na sasa inasubiri mshindi kati ya Yanga na Azam FC.
Wekundu wa Msimbazi wametinga fainalj kwa kishindo baada ya ushindi mnono wa mabao 4-0 mbele ya Coastal Union, mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abedi mjini Arusha.
Katika nusu fainali hiyo, Libasse Gueye aliitanguliza Simba kwa bao la dakika ya 19, kabla ya Nickson Kibabage kuongeza jingine (Dk. 59).
Wakati Coastal wakidhani kazi imeishia hapo, beki wa kati wa Coastal, Rushine De Reuck, aliongeza dakika ya 77, kabla ya Clatous Chama naye kuingia kambani (Dk. 80).
Yanga watakuwa dimbani kesho kuikabili Simba katika nusu fainali itakayochezwa katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.


