20.5 C
New York

Haiti yatangulia kung’oka Kombe la Dunia 2026

Published:

NEW YORK, Marekani

TIMU ya soka ya Taifa ya Haiti imekuwa ya kwanza kuaga msimu huu wa fainali za Kombe la Dunia zinazofanyika Marekani, Mexico na Canada.

Haiti haina cha kupambania baada ya mechi zao mbili, safari hii ikifungwa mabao 3-0 na Brazil katika mchezo wa alfajiri ya leo.

Cunha alifunga mabao mawili ndani ya dakika 13, kabla ya Vinicius Junior kufunga na kufikisha mabao mawili ya Kombe la Dunia.

Brazil sasa wanaisubiri Scotland ambayo imetoka kupoteza mbele ya vigogo wa soka la Afrika, Morocco.

Habari ya Haiti kutolewa imekuja zikiwa ni siku chache tu zimepita tangu Mexico ilipoweka rekodi ya kuwa timu ya kwanza kuvuka makundi na kuingia hatua ya 32 Bora.

Related articles

Recent articles