Na mwandishi wetu, Gazetini
TAKWIMU za sasa, kwa mujibu wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP), uchafuzi wa mazingira umeongezeka kwa kasi katika maeneo mengi duniani.
Ni kwa mujibu wa takwimu zilizopo, jumla ya tani milioni 460 ya takataka za plastiki zilizalishwa kwa mwaka 2025 pekee.
Aidha, ripoti yake ya Upotevu wa Vyakula, UNEP inaonesha kuwa uzalishaji wa bidhaa za plastiki uliongezeka kutoka tani milioni 234 mwaka 2000 hadi tani milioni 460 mwaka 2019.
Wakati huo huo, inaonekana kuwa takataka zinazotokana na vyakula zimezalishwa kwa kiwango cha tani bilioni 1.05. Kiwango hicho ni asilimia 19 ya vyakula duniani.
Katika ripoti ya UNEP, inaelezwa kuwa kiwango kikubwa cha takataka za vyakula kinazalishwa majumbani, ambacho ni takribani tani milioni 631 kwa mwaka.
Wakati kiwango cha takataka hizo kikiwa kikubwa kwa kiasi hicho, watu zaidi ya milioni 780 wanapitia janga la njaa katika maeneo mbalimbali duniani.


