5.7 C
New York

Libya iliyogawanyika na mateso wanayopitia wanawake

Published:

TRIPOLI, Libya

MATUKIO ya wanawake watatu kuuawa yamezua mjadala mkubwa juu ya usalama jinsia hiyo nchini Libya.
Staa wa mitandao ya kijamii, Khansa Al-Mujahid, aliuawa kwa kupigwa risasi akiwa kwenye gari lake mjini Tripoli.

Kama hiyo haitoshi, mwanamke mwingine, Amani Hajja, alishitua wengi kwa taarifa za kifo chake mjini Misrata. Amani aliuawa na ndugu zake, na kisha mwili wake kutupwa mtoni huko Kusini-Maahariki mwa Tripoli.

Lakini, ukiacha mauaji, wanawake nchini Libya wamekuwa wakipitia changamoto nyingi, ikiwamo kunyimwa haki za kisiasa, kiuchumi na kijamii.

Asma Khalifa ni mtetezi wa haki za wanawake na muasisi wa Taasisi ya Tamazight Women’s Movement.
“Libya haina sheria zinazomlinda mwanamke na hata kama zingekuwepo, hakuna polisi wa kuhakikisha zinafuatwa.”

Kwa upande wake, Ali Omar, ambaye ambaye pia ni mtetezi wa haki za binadamu kupitia Taasisi yake ya Libya Crimes Watch, anasema: “Uonevu dhidi ya wanawake si jambo geni au la ghafla (nchini Libya). Kiwango cha ukatili dhidi yao kimekuwa kikubwa kwa miaka mingi.”

Omar mwenye makazi yake jijini London, Uingereza, anafichua kuwa wanawake wamekuwa wakishindwa kuripoti juu ya unyanyasaji wakihofia kukiuka maadili ya jamii au mafundisho ya dini.

Wakati huo huo, kukosekana kwa Serikali kuu tangu Muammar Gaddafi alipotolewa madarakani mwaka 2011 nako kunatajwa kuwa chanzo cha mateso wanayopitia wanawake kwa sasa.

Miaka mitatu baada ya utawala wa Gaddafi kuangushwa, Libya iligawanyika na kuzalisha Serikali mbili.
Kwa upande mmoja, ipo Serikali inayoongozwa na Waziri Mkuu, Abdul Hamid Dbeibah, ambayo ndiyo inayotambuliwa na Umoja wa Mataifa (UN) na makao makuu yake yako Mji Mkuu, Tripoli.

Ukienda Mashariki mwa Mji wa Benghazi, ipo Serikali pia na inaongozwa na Waziri Mkuu, Ossama Hammad.
Pande zote mbili za Serikali, kwa maana ya Tripoli na Benghazi, kila moja ina washirika wake wa nje na vikundi vya waasi vya ndani ya Libya.

Ni kutokana na mazingira hayo ya uhasimu, vikundi vya kijeshi kutoka Serikali zote mbili navyo vimekuwa vikinufaika kwa kuwafanyia ukatili wanawake na wasichana. “Kwa sasa, ni kawaida sana kwa mwanamke kukubali kuolewa na wapiganaji ili kuepuka ugumu wa maisha,” anasema mwanaharakati Asma Khalifa.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img