2.8 C
New York

Kombe la Dunia 2026; Kundi I

Published:

Na mwandishi wetu, Gazetini

KUMEKUCHA! Droo ya hatua ya makundi ya fainali za Kombe la Dunia ilichezeshwa nchini Marekani.
Kwa mara ya kwanza, fainali hizo zitashirikisha mataifa 48, huku mechi 104 zikitarajiwa kuchezwa katika viwanja mbalimbali vya Marekani, Mexico na Canada.

Tukijikumbushe; timu 42 zilishakata tiketi na sasa zinasubiriwa zingine sita zitakazopatikana kupitia mechi za ‘play-off’ zitakazochezwa Machi, mwakani. Sasa, makala haya yanaliangazia Kundi I na kuchambua timu zilizopo kuelekea michuano hiyo itakayoanza Juni 11, mwakani.

Katika Kundi hili, zipo Ufaransa, Senegal, Norway na timu moja itakayofuzu kupitia ‘playoff’ kati ya Bolivia, Suriname na Iraq. Uhondo wa Kundi hili ni kuwaona Kylian Mbappe (Ufaransa) na Erling Haaland (Norway) wakikutana katika moja ya mechi za hatua ya makundi.

Pia, Ufaransa wanakumbuka waliyowahi kufungwa bao 1-0 na Senegal katika mechi ya kwanza ya fainali za mwaka 2002. Norway, licha ya kwamba wanaweza kubezwa, walifuzu wakiwa hawajapoteza mchezo. Pia, ndiyo timu iliyofuzu ikiwa na mabao mengi ya kufunga (37) barani Ulaya.

Senegal iko chini ya kocha mzawa, ambaye ni nyota wao wa zamani, Pape Thiaw. Ukiacha Sadio Mane katika eneo la ushambuliaji, safu ya kiungo ina Ismaïla Sarr, Pape Matar Sarr, Habib Diarra na Iliman Ndiaye.
Je, ni ipi kati ya Bolivia, Suriname na Iraq itakayoongezeka na kulifanya Kundi hili kutimiza idadi ya timu nne?

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img