21.2 C
New York

Yametimia! Waziri Mkuu Uingereza abwaga manyanga

Published:

LONDON, Uingereza

BAADA ya tetesi za muda mrefu, hatimaye Waziri Mkuu wa Uingereza, Keir Starmer, ametangaza kujiuzulu.

Kwa wiki kadhaa za hivi karibuni, Starmer amekuwa kwenye shinikizo la kujiuzulu hata kutoka ndani ya Chama chake cha Labour.

Katika hotuba yake ya kujiuluzu leo Juni 22, 2026, Waziri Mkuu huyo amesema uamuzi wake umetokana na mapenzi makubwa aliyonayo kwa nchi yake.

Aliongeza pia, anamshukuru mke wake, Vic, akimtaja kuwa ni mwamba. Amesisitiza kuwa anataka kuwa karibu na watoto wake.

Kwa upande mwingine, Starmer amesisitiza kuwa ataendelea kukiongoza Chama, Labour, hadi pale atakapochaguliwa kiongozi mwingine.

Related articles

Recent articles