Na mwandishi wetu, Gazetini
CHINA ndiyo nchi inayoongoza kwa matumizi ya kiwango kikubwa cha umeme duniani, ikifuatiwa na Marekani, India na Urusi, kwa mujibu wa tovuti ya takwimu ya Ember.
Katika takwimu, Taifa hilo la barani Asia lilitumia TWh 10,573 kwa mwaka 2025, sawa na theluthi ya matumizi yote duniani kwa kipindi hicho.
Aidha, ongezeko hilo ni asilimia 10 ya matumizi ya nishati hiyo nchini China, ikilinganishwa na takwimu za miaka ya 2000.
Wakati huo huo, kiwango hicho cha China ni kikubwa kuliko jumla ya matumizi ya umeme katika mataifa ya Marekani, India, Urusi na Japan.
Kwa Marekani inayoshika nafasi ya pili, matumizi yake ya umeme kwa mwaka 2025 ni TWh 4,536, ikifuatiwa na India (TWh 2,083) na Urusi (TWh 1,176).
Mataifa mengine kwenye ‘Top 10’ ni Japan (TWh 1,030), Brazil (TWh 762), Canada (TWh 646), Korea ya Kusini (TWh 646), Ujerumani (TWh 520), na Ufaransa (TWh 477).


