TEHRAN, Iran
BAADA ya Rais wa Marekani, Donald Trump, kudai kuwa mazungumzo ya kumaliza vita yao na Iran yako kwenye hatua za mwisho, uongozi wa Taifa hilo la Kiarabu umekuja na mtazamo tofauti.
Kwa mujibu wa Iran, hakuna chochote cha maana kilichofikiwa hadi sasa, hivyo anachokisema Rais Trump si sahihi.
Katika taarifa yake ya awali, alisema amegiza jeshi la Marekani kusitisha mashambulizi zaidi nchini Iran baada ya hatua kubwa iliyofikiwa na wasuluhishi wa mgogoro huo.
Rais Trump alidai kuwa hatua iliyobaki sasa ni kusainiwa kwa nyaraka tu, kisha vita hivyo vimalizike ndani ya siku chache zijazo. Aliahidi pia sherehe ya kumaliza mgogoro itakayofanyika Ulaya.
Hata hivyo, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, Esmail Baghaei, amesema hakuna kilichofikiwa hadi sasa katika kumaliza vita hivyo vilivyoanza Februari 28, 2026.


