WASHINGTON DC Marekani
UTAFITI mpya umonesha kuwa ushawishi wa Marekani kwa mataifa ya Ulaya imeporomoka kwa kiasi kikubwa tangu Rais Donald Trump aliporejea madarakani mwaka 2024.
Kwa mujibu wa utafiti huo, kwa sasa ni asilimia 11 tu ya raia wa nchi za Umoja wa Ulaya (EU) wanaoiamini na kuichukulia Marekani kama mshirika wao.
Ni tofauti na miezi sita iliyopita, ambapo utafiti wa Baraza la Mahusiano ya Kimataifa la Umoja huo (ECFR) ulionesha kuwa asilimia 16 ya raia wa mataifa ya Ulaya walikuwa na mtazamo chanya na Marekani.
Pia, matokeo ya utafiti wa sasa yanakinzana na ule wa Novemba, 2024, wakati Trump anaingia madarakani, ambapo asilimia 22 waliitaja Marekani kama mshirika sahihi.
Aidha, utafiti wa safari hii unakuja wakati zikiwa zimebaki wiki chache kabla ya kufanyika kwa mikutano mikubwa miwili ya G7 na NATO.
Kwa upande mwingine, wachambuzi wa siasa wanaona kushuka kwa ushawishi wa Marekani barani Ulaya kumetokana na sera za Rais Trump.


