18.4 C
New York

Kwa mastaa hawa, pesa siyo shida zao kabisa

Published:

NAIROBI, Kenya

KWA miaka mingi, wanamuziki wa Kenya wamekuwa wakifanya vizuri kwa Ukanda huu wa Afrika Mashariki, licha ya upinzani mkali kutoka kwa wenzao wa Tanzania na Uganda.

Kutokana na kazi zao kufanya vizuri sokoni, pia harakati zingine za nje ya sanaa, haishangazi kuona baadhi ya wanamuziki wa Kenya wakiishi kifalme kutokana na pesa ndefu wanazovuna.

AKOTHEE

Jina la ‘Madam Boss’ limetokana na mkwanja mrefu alionao bibiye huyo. Akothee, ambaye jina halisi ni Esther Akoth, anatajwa na tovuti ya Fineducke kuwa ana utajiri wa Ksh bilioni moja (zaisi ya Sh bil. 20 za Tanzania).

Akothee (42), hategemei muziki peke yake, bali pia anavuna fedha nyingi katika biashara zake, ikiwamo ya kuuza na kupangisha nyumba. Pia, anamiliki kampuni za usafirishaji.

PREZZO

Wengi wanamwita hivyo lakini jina lake halisi ni Jackson Ngechu Makini na ana umri wa miaka 45. Kwa mujibu wa tovuti ya Fineducke, rapa huyo ana utajiri wa Ksh milioni 650 (zaidi ya Sh bil. 13 za Tanzania).

Mbali ya muziki na dili za matangazo, Prezzo ambaye ni miongoni mwa wanamuziki wa muda mrefu kwenye gemu, ana biashara zake zinazompa mkwanja wa kutosha.

JAGUAR

Kwa wasiomfahamu, jina lake halisi ni Charles Njagua Kanyi. Umri wake ni miaka 39 na kwa sasa anatajwa kuwa na utajiri wa Ksh milioni 500 (zaidi ya Sh bil. 10 za Tanzania).

Nje ya muziki, ambao pia umempa fedha nyingi, mshikaji ni bosi wa kampuni za kuuza na kupangisha nyumba. Wakati huo huo, amewekeza katika sekta ya usafirishaji, ambayo inamlipa vizuri.

KRG THE DON

Jina alilopewa na wazazi ni Karuga Kimani. KRG The Don anafahamika kwa maisha yake ya ‘kula bata’, hiyo ikitokana na utajiri wake wa Ksh milioni 400 (zaidi ya Sh bil. 8 za Tanzania).

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 34, kama ilivyo kwa wasanii wengine wenye pesa ndefu, amekuwa kwenye biashara ya kuuza na kupangisha nyumba.

NONINI

Wanaomfahamu vizuri wanamwita Hubert Mbuku Nakitare. Ndilo jina lake halisi. Nonini ni miongoni mwa malejendari wa muziki nchini Kenya na sasa utajiri wake ni Ksh milioni 210 (zaidi ya Sh bil. 4.2 za Tanzania).

Akiwa na umri wa miaka 42, amekuwa akivuna pesa ndefu SI tu kwenye muziki, bali pia dili za matangazo, mialiko katika hafla, bila kusahau ana biashara zake nyingi.

BAHATI

Kevin Mbuvi Kioko, maarufu kwa jina la Bahati, alianzia katika gospo, kabla ya kujitosa kwenye muziki wa dunia. Ana umri wa miaka 31 tu lakini tayari ana utajiri wa Ksh milioni 200 (Sh bil. 4 za Tanzania).

Mbali ya biashara zingine, Bahati amekuwa akivuna pesa ndefu kupitia ngoma zake, dili za matangazo na kipindi chake cha runinga cha ‘The Bahati’s Empire).

KHALIGRAPH JONES

Mmoja ya wasanii bora wa muziki wa Hip hop kwa Ukanda huu wa Afrika Mashariki na Kati. Jina lake halisi ni Jane Nyambura na umri ni miaka 35.

Khaligraph, pia akifahamika kwa jina la ‘Papa Jones’, anatajwa kuwa na utajiri wa Ksh milioni 190 (zaidi ya Sh bil. 3.4) kutokana na muziki na ishu zake zingine.

OCTOPIZZO

Utajiri wa Ksh milioni 160 (zaidi ya Sh bil. 3.2 za Tanzania). Henry Ohanga, jina halisi alilopewa na wazazi wake, ana umri wa miaka 37, akiwa miongoni mwa marapa tishio nchini Kenya na Afrika Mashariki kwa ujumla.

Kwa Kenya, mbali ya muziki, anafahamika kwa harakati zake za kuwapigania vijana. Sehemu ya fedha zake hupatikana pia katika biashara anayofanya nje ya gemu.

Related articles

Recent articles