21.9 C
New York

Mel B kuirudisha Spice Girls miaka 30 ya ngoma yao

Published:

LOS ANGELES, Marekani

MEMBA wa Kundi la Spice Girls, Mel B, amesema watafanya jambo kwa ajili ya kumbukizi ya miaka 30 ya wimbo wao uliowahi kufanya vizuri katika soko la muziki duniani, ‘Wannabe’.

Mel B (51), ambaye mashabiki wake wanamfahamu pia kwa jina la Scary Spice, alikuwa sehemu ya kundi hilo, sambamba na Victoria Beckham, Melanie Chisholm, Emma Bunton na Geri Halliwell-Horner.

Wimbi wao huo, Wannabe, ulitoka mwaka 1996 na kuteka vituo vya redio na televisheni vya ndani na nje ya Marekani.

Baadaye, Kundi hilo liliendelea kuteka dunia kwa ngoma zake nzuri, zikiwamo ‘Who Do You Think You Are?’ na ”Stop and Viva Forever’.

Hata hivyo, likiwa kwenye kilele cha mafanikio, Kundi hilo lilivunjika Desemba, 2000, liha ya jitihada za hapa na pale za kulirejesha.

Related articles

Recent articles