32 C
New York

Staa Nigeria apoteza uwezo wa kuona

Published:

LAGOS, Nigeria

MWANAMUZIKI maarufu wa Nigeria, Remi Aluko, amefichua kuwa macho yake yamepoteza uwezo wa kuona.

Katika mahojiano yake na kituo cha runinga cha Oyinmomo, amesema amekuwa akisumbuliwa na tatizo la macho kwa miaka mingi.

Aluko amedai kuwa hali imekuwa mbaya zaidi baada ya kufanyiwa upasuaji, akisema kwa sasa hana tofauti na kipofu.

Kwa upande mwingine, msanii huyo amesema hali yake hiyo haijamkatisha tamaa ya kuendelea na kazi zake. “… Licha ya kutokuona, wengi hawajui kwa sababu sitaki hali yangu inivunje moyo,” amesema.

Staa huyo anafahamika kuwa ni shabiki mkubwa wa Wizkid, ambaye amekuwa akimtaja kuwa ni msanii aliyeleta mapinduzi makubwa katika soko la muziki nchini Nigeria.

Related articles

Recent articles