LAGOS, Nigeria
STAA wa muziki nchini Nigeria, Chinedu Okoli, maarufu kwa jina la Mr Flavour, ameweka wazi kuwa ni ngumu kwake kuwa kwenye mahusiano na mwanamke mmoja.
Flavour anafahamika kuwa ni baba wa watoto watatu aliowapata katika mahusiano na wanawake watatu tofauti.
Akizungumzia hilo, staa huyo amesema yeye ni wa ‘dunia tofauti’ kwani si mwanaume mwenye utamaduni wa kutulia kwenye mapenzi.
“Mimi ni mzuriraji. Niko kwenye dunia ya ajabu sana. Mimi ni mtoto wa kitaa. Wanaume wengine wametulia, lakini siyo mimi. Siwezi kujifungia kwenye chumba,” amesema.
Nyota huyo ana ngoma nyingi zinazofanya vizuri, ikiwamo ‘Nabania’, iliyompa mashabiki wengi ndani na nje ya Afrika.


