13.5 C
New York

Gallas: Simeone ataipa mataji Chelsea

Published:

LONDON, Uingereza

BEKI wa kati wa zamani wa Chelsea, William Gallas, anaamini Diego Simeone ndiye kocha sahihi wa kupewa mikoba ya kuinoa timu hiyo.

Chelsea wanahitaji kocha mpya kwa ajili ya msimu ujao baada ya kumfuta kazi Liam Rosenior.

Gallas, ambaye pia aliwahi kukipiga Arsenal, amesema Simeone anayeinoa Atletico Madrid ni kocha mwenye morali ya makombe.

“Kama ni kwa ajili ya mipango ya muda mfupi, basi wanamuhitaji Diego Simone kutokana na sifa yake. Anaweza kuwapa mataji ndani ya muda mfupi,” amesema.

Wakati huo huo, Gallas raia wa Ufaransa amesema si vibaya pia endapo Blues watampa ajira Cesc Fabregas.

Wawili hao walicheza Pamoja Arsenal na sasa Fabregas anainoa Como ya Ligi Kuu ya Italia (Serie A).

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img